Shirika la ndege la Tanzania (ATCL) limezindua safari za ndege ya moja kwa moja kutoka Dar es Salaam hadi Accra nchini Ghana.
Kulingana na Waziri wa Uchukuzi wa Tanzania, Makame Mbarawa, hatua hiyo ni sehemu ya maandalizi ya Kombe la mataifa ya Afrika (AFCON 2027), ambayo itaandaliwa kwa pamoja na Tanzania, Kenya na Uganda.
Ili kurahisisha maandalizi ya AFCON 2027, Mbarawa alisema kuwa kutakuwa na ndege tatu za kila wiki, kati ya Dar es Salaam na Accra, ili kuimarisha uhusiano wa kiuchumi, na kurahisisha usafiri kati ya Afrika Mashariki na Magharibi.