
Katika taarifa iliyotoa leo, Mamlaka ya Israel inayosimamia masuala ya kiraia katika maeneo ya Palestina, COGAT, imesema kivuko hicho cha Rafah kitafunguliwa kwa pande zote mbili na kwamba kuingia na kutoka kutaruhusiwa kwa ushirikiano na Misri kufuatia uchunguzi wa awali wa kiusalama wa watu binafsi utakaofanywa na Israel, chini ya usimamizi wa ujumbe wa Umoja wa Ulaya.
Kivuko hicho kilichoko kusini mwaGazakatika mpaka wake na Misri, ndio njia ya pekee ya kuingia na kutoka Gaza isiyopitia Israel.