Katika taarifa yake, jeshi hilo limesema limewatambua magaidi wanane walioibuka kutoka maficho ya chini ya ardhi na kwamba jeshi la anga liliwalenga na kuwauwa watatu.

Bila kutoa maelezo yoyote kuhusu utambulisho wa walengwa wake, limesema mashambulizi yalifanywa na maafisa wake wanaendelea kufanya msako katika eneo hilo ili “kuwaangamiza magaidi wote.”

Jeshi hilo limeongeza kuwa vikosi vyake vitaendelea kusalia katika eneo hilo kulingana na makubaliano ya kusitisha mapigano na vitaendelea kufanya kazi ili kukabiliana na tishio lolote.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *