
Katika taarifa kupitia televisheni ya taifa jana jioni, Tchiani alitoa tahadhari kwa wafadhili wa makundi hayo aliyoyaita ya mamluki kuwa itachukuwa hatua za kisasi.
Hata hivyo hakutoa ushahidi wowote wa kuunga mkono madai yake.
Video zinazoonekana kutoka eneo la tukio zilinasa milipuko mikubwa iliyoanza mwendo wa saa sita usiku na kudumu kwa takriban masaa mawili katika eneo la Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Diori Hamani huko Niamey.