Katika mkutano na waandishi wa habari leo akiwa na mwenzake wa Iran Abbas Araghchi mjini Istanbul, Fidan amesema  wanaona kwamba Israel inajaribu kuishawishi Marekani kuanzisha mashambulizi ya kijeshi dhidi ya Iran.

Ameongeza kuwa juhudi hizo zina uwezo wa kuharibu kabisa uthabiti unayoyumba wa kanda yao na kwamba anatumaini Marekani itatumia busara na kutoruhusu hilo kutokea.

Fidan amesema kuanza tena kwa mazungumzo ni muhimu ili kuepusha vita vibaya.

Vyombo vya habari vya Uturuki vimeripoti kuwa Rais Tayyip Erdoğan amependekeza mazungumzo ya ngazi ya juu ya pande tatu na Rais wa Marekani Donald Trump na Iran ili kutuliza mzozo huo.

Araghchi amethibitisha kuwa Iran iko tayari kwa mazungumzo lakini kwa “masharti ya haki na usawa,” huku akisisistiza kuwa nchi yake inakataa mazungumzo yoyote juu ya uwezo wake wa ulinzi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *