Halmashauri ya Jiji la Mbeya inatarajia kuanzisha kituo maalumu cha kutunza watoto katika soko la Mwanjelwa, kitakachogharimu zaidi ya shilingi milioni 92.
Ili kufanikisha mpango huu, tayari imeanzishwa harambee ya kuchangia ujenzi wa kituo hicho, ambacho kitalinda watoto kutokana na ajali na kuzurura hovyo mitaani, huku wakiwa na nafasi salama na malezi bora wakati wazazi wao wanajishughulisha na biashara.
#AzamTVUpdates
✍Kakuru Msimu
Mhariri | John Mbalamwezi
(Feed generated with FetchRSS)