Ali Larijani, Katibu wa Baraza Kuu la Usalama wa Taifa la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, amekutana na kufanya mazungumzo na Rais Vladimir Putin wa Russia mjini Moscow.

Kulingana na ripoti ya Russia Today Ijumaa usiku, msemaji wa Kremlin Dmitry Peskov alitangaza kwamba Rais wa Russia alimkaribisha Katibu wa Baraza Kuu la Usalama wa Kitaifa la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran mjini Moscow kwa ajili ya mazungumzo.

Hakuna maelezo zaidi kuhusu mkutano huo na masuala yaliyojadiliwa ambayo yametolewa hadi sasa.

Kazem Jalali, Balozi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran nchini Russia, ametangaza kwamba Ali Larijani, Katibu wa Baraza Kuu la Usalama wa Taifa la Iran, Ijumaa jioni alikutana na kuzungumza na Rais wa Russia Vladimir Putin.

Hata hivyyo imeelezwa kuwa, lengo kuu la mazungumzo hayo lilikuwa ni kupanua uhusiano wa pande mbili, hasa uhusiano wa kiuchumi kati ya nchi hizo mbili, na wakati huo huo, pande hizo mbili zilijadili masuala muhimu ya kikanda na kimataifa.

Vyombo vya habari vya Russia vimetangaza kwamba madhumuni ya mkutano wa Larijani na Putin ni kujadili matukio ya kikanda na masuala ya pande mbili.

Kwa mujibu wa ripoti za vyombo mbalimbali vya habari, mazungumzo kati ya Rais Vladimir Putin na Ali Larijani Katibu wa Baraza Kuu la Usalama wa Taifa la Iran yanachukuliwa kuwa na maana kubwa katika hali nyeti ya hivi sasa katika eneo hili na vitisho vya Marekani, na sambamba na makubaliano ya kimkakati kati ya nchi hizo mbili katika nyanja za kijeshi na usalama.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *