
Kwa mujibu wa maafisa wa hospitali zilizopokea miili ya marehemu siku moja baada ya Israel kuishutumu Hamas kwa kukiuka masharti mapya ya usitishaji mapigano, mashambulizi yalilenga maeneo mbalimbali ya Gaza, ikiwemo mashambulizi kwenye jengo la ghorofa mjini Gaza na kambi ya mahema huko Khan Younis. Na kwa mujibu wa mkurugenzi wa Hospitali ya Shifa, Mohamed Abu Selmiya miongoni mwa waliouawa ni wanawake wawili na watoto sita kutoka familia mbili tofauti.Shambulio la angani pia lililenga kituo cha polisi mjini Gaza, na kuua takriban watu 14 na kuwajeruhi wengine kadhaa. Mashambulizi ya Jumamosi yanakumbusha kwamba idadi ya vifo Gaza bado inaongezeka licha ya makubaliano ya usitishaji mapigano kuendelea kusogea hatua kwa hatua.