#HABARI: Mbunge wa Jimbo la Lupa, Mhe. Masache Njelu Kasaka, amebainisha kuwa maadhimisho ya miaka 49 ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) ni kielelezo cha mafanikio makubwa ya kimaendeleo yaliyofikiwa nchini na ndani ya jimbo lake.
Akizungumza katika uzinduzi wa sherehe hizo zilizofanyika Kata ya Lupa, wilayani Chunya, Mhe. Kasaka alitaja ufunguzi wa barabara, uboreshaji wa miundombinu ya elimu na afya, pamoja na kukua kwa sekta za uchimbaji madini na kilimo cha tumbaku kama faida za utekelezaji wa ilani ya chama hicho.
Mhe. Kasaka alisisitiza kuwa mabadiliko yanayoonekana sasa katika utoaji wa huduma kwa jamii ni tofauti kabisa na miaka ya nyuma, jambo linalothibitisha kuwa CCM inatimiza ahadi zake kwa wananchi.
Sherehe hizo, zilizohudhuriwa na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Mbeya, Bw. Patrick Mwalunenge kama mgeni rasmi, zimetumika kama jukwaa la kuonyesha namna chama hicho kinavyoendelea kuleta mabadiliko ya kiuchumi na kijamii jimboni Lupa na taifa kwa ujumla.
Powered by #MCHEZOSUPA
JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:
–
Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.
#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
#Follow @itvtz @radioonetanzania
@capitaldigitaltanzania.