#HABARI: Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) mkoani Mtwara unatarajia kusajili bure kaya 38,000 zisizojiweza ili kunufaika na huduma za afya, huku kipaumbele kikielekezwa kwenye kaya laki mbili na nusu.

Meneja wa mkoa huo, Dkt. Edwin Chitage, ameeleza kuwa baada ya kukamilisha usajili wa kaya hizo, awamu ya pili itawahusu wananchi wengine watakaotakiwa kulipia shilingi 150,000 kwa ajili ya wanufaika sita, zoezi litakalotekelezwa kwa ushirikiano wa viongozi kuanzia ngazi ya mkoa hadi vijiji.

Wakati NHIF ikijipanga kutoa elimu kwa jamii kuhusu usajili huo, baadhi ya wananchi mkoani Mtwara wametoa wito kwa Serikali kuhakikisha kuwa mpango wa bima ya afya kwa wote unaambatana na upatikanaji wa uhakika wa dawa na vipimo.

Dkt. Chitage amesisitiza kuwa ofisi yake imejipanga vema kutoa elimu kuanzia ngazi ya mitaa ili kuhakikisha wananchi wanaelewa manufaa ya bima hiyo na kupata huduma bora bila ubaguzi.

Powered by #MCHEZOSUPA

JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:

Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.

#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
#Follow @itvtz @radioonetanzania
@capitaldigitaltanzania.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *