#HABARI: Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Edward Mpogolo, ameongoza zoezi la usafi katika fukwe ya Dengu jijini Dar es Salaam, huku akikemea vikali utupaji wa taka hovyo, hususan chupa za plastiki, kwenye mito na mitaro.
Mpogolo amebainisha kuwa taka hizo husafirishwa hadi baharini na kuhatarisha afya ya binadamu pamoja na viumbe wa majini, jambo lililopelekea ushirikiano na Shirika la JUZA katika kuimarisha uhifadhi wa mazingira.
Aidha, Mpogolo amesisitiza kuwa serikali imejipanga kuboresha hali ya usafi katika fukwe za jiji hilo ili kukuza sekta ya utalii na kuvutia wageni zaidi. Zoezi hilo limeungwa mkono na wadau mbalimbali wa mazingira, akiwemo Dkt. Erick Mwate na Mariam Lulida, ambao wamehimiza jamii kubadili tabia ili kulinda rasilimali za bahari kwa faida ya vizazi vya sasa na vijavyo.
Powered by #MCHEZOSUPA
JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:
–
Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.
#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
#Follow @itvtz @radioonetanzania
@capitaldigitaltanzania.