#HABARI: Spika Mstaafu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Kamisaa wa Sensa ya Watu na Makazi ya mwaka 2022, Mheshimiwa Anna Makinda, amesema kuwa mafanikio ya mwanafunzi akiwa shuleni yanategemea nidhamu, bidii katika kujifunza na uwezo wa kujiongoza tangu akiwa katika ngazi ya chini.
Mheshimiwa Makinda ameyasema hayo alipokuwa akizungumza katika hafla maalum iliyowakutanisha wanafunzi waliowahi kusoma katika Shule ya Sekondari ya Masasi Girls, iliyokuwa awali ikijulikana kama Salvatorian Secondary School.
Ameeleza kuwa nidhamu ni msingi muhimu wa elimu, akisisitiza kuwa mwanafunzi anayejijengea maadili mema mapema huwa na uwezekano mkubwa wa kufanikiwa siyo tu kitaaluma bali pia katika maisha ya baadaye.
Mheshimiwa Makinda amewahimiza wanafunzi waliopo na wahitimu wa shule hiyo kuendelea kuthamini elimu, kufanya kazi kwa bidii na kuzingatia maadili mema ili kuwa raia wenye mchango chanya kwa jamii na Taifa kwa ujumla.
Powered by #MCHEZOSUPA
JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:
-
Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.
#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
Follow @itvtz @radioonetanzania
@capitaldigitaltanzania.