Chanzo cha picha, TASNIMNEWS
Mohammad Baqer Qalibaf, Spika wa Bunge la Iran amesema katika kikao cha hadhara hii leo: “Kwa mujibu wa kifungu cha 7 cha sheria kuhusu hatua za kukabiliana na tangazo la IRGC kuwa ni shirika la kigaidi, majeshi ya nchi za Ulaya yanahesabiwa kuwa ni makundi ya kigaidi, na matokeo ya hatua hiyo yatakuwa jukumu la Umoja wa Ulaya.”
Bw. Qalibaf alisema: “Wazungu walijipiga risasi miguuni kwa kujaribu kuipiga IRGC, ambayo ilikuwa kikwazo kikubwa cha kuenea kwa ugaidi Ulaya.”
Kulingana na yeye, “hatua ya kutowajibika” ya Umoja wa Ulaya ilikuwa “kufuata maagizo ya Rais wa Marekani” na Israel, ambayo “itaharakisha njia ya Ulaya ya kutokuwa na umuhimu katika utaratibu wa ulimwengu ujao.”
Umoja wa Ulaya ulitangaza Alhamisi, Januari 29, kwamba umeliorodhesha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC) kama shirika la kigaidi.
Hatua ya hivi majuzi ya Umoja wa Ulaya imeibua hisia kali kutoka kwa maafisa wengi wa Jamhuri hiyo ya Kiislamu.