Katika kuendeleza hamasa ya kitaifa ya uwekezaji wa ndani, Mamlaka ya Uwekezaji na Maeneo Maalumu ya Kiuchumi Tanzania (TISEZA) imetembelea mradi wa Hospitali ya Kamanga Medics (Kamanga Medics Hospital) uliopo eneo la Nyegezi jijini Mwanza, ambao kwa sasa uko katika hatua ya upanuzi.

Hospitali hiyo inayotarajiwa kutoa ajira za moja kwa moja kwa wafanyakazi kati ya 350 hadi 380 wa kudumu, imesajiliwa rasmi na TISEZA huku ikikidhi vigezo vya kupewa vivutio mbalimbali, vikiwemo vya kikodi na visivyo vya kikodi.

✍Upendo Michael
#AzamTVUpdates
Mhariri | John Mbalamwezi

(Feed generated with FetchRSS)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *