
Hiki ni kipindi kinachohusisha mahojiano ya kusisimua na wageni mbalimbali kutoka ndani na nje ya Japani.
Wakati huu tunakuletea kipindi cha Tupike Kijapani ambapo tutapika pamoja chakula cha “chan chan yaki,” chakula chenye samoni wa mwituni na samaki aina nyingine.
Ni mapishi ya kitamaduni kutoka mkoani Hokkaido
Aidha, utasikiliza namna watangazaji wetu wanavyozamia gumzo za kuvutia zitakazokuacha ukivunjika mbavu. Pia tutasoma ujumbe wako msikilizaji. Usikose kusikiliza!