Waziri wa Ulinzi wa Korea Kusini Ahn Gyu-back ameishukuru Japani kwa kusaidia ndege ya kijeshi ya Korea Kusini iliyokumbwa na matatizo. Ndege ya usafiri ya C-130 ililazimika kutua kwa dharura katika Mkoa wa Okinawa.

Ndege hiyo ilitua majira ya saa 5 asubuhi Januari 30 katika Kambi ya Kikosi cha Kujihami cha Anga cha Japani cha Naha. Ilikuwa ikielekea Saudi Arabia kwa maonyesho ya kimataifa ya ulinzi wakati uzalishaji mdogo wa injini ulipogunduliwa.

Mafundi walibadilisha vipuri vyenye kasoro na ndege ikaondoka Japani kabla ya saa moja jioni.

Waziri wa Ulinzi wa Japani Koizumi Shinjiro alikutana na mwenzake wa Korea Kusini katika Mkoa wa Kanagawa kusini mwa Tokyo Januari 30 muda wa mchana. Ahn alitoa shukrani kwa msaada wa Japani katika kushughulikia tukio hilo.

Mawaziri hao wawili pia walikubaliana kukuza ushirikiano zaidi wa ulinzi.

Jeshi la Anga la Korea Kusini lilipata msaada wa mafuta kutoka ASDF nchini Japani kwa mara ya kwanza Januari 28, wakati kundi la ndege la wakufunzi aina ya T-50 lilipotua Okinawa.

Mwezi Julai, ndege ya kijeshi ya usafiri ya Korea Kusini iliingia katika eneo la utambuzi wa ulinzi wa anga la Japani bila taratibu zinazofaa wakati wa kutua kwa dharura katika Kambi ya Kadena ya jeshi la Marekani huko Okinawa.

Japani ilirusha ndege za kivita kwa kasi ili kujibu, na kuihimiza Korea Kusini kuzuia hilo kutokea tena.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *