Mazungumzo ya amani ya pande tatu yanayohusisha Ukraine, Urusi na Marekani yanatarajiwa kuanza tena Februari Mosi yakizingatia suala la eneo.
Maafisa wa ngazi za juu kutoka nchi hizo tatu walifanya mkutano wao wa kwanza wa kukomesha vita nchini Ukraine kwa muda wa siku mbili hadi Januari 24 huko Abu Dhabi, mji mkuu wa Falme za Kiarabu.
Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskyy alisema mazungumzo hayo yalijumuisha masuala mbalimbali ya kijeshi yanayohitajika ili kukomesha vita.
Upande wa Urusi ulielezea mazungumzo hayo kama yanayofanyika katika “mazingira yenye kuleta tija.”
Hata hivyo, Urusi na Ukraine zinaonekana kutofautiana kuhusu suala la eneo. Urusi inataka kuondolewa kwa wanajeshi wa Ukraine kutoka eneo la mashariki la Donbas, ambalo Urusi imelichukua, pendekezo ambalo Ukraine inaona ni vigumu kukubali.
Shirika la habari la Reuters linaripoti kwamba mjumbe maalum wa Rais Vladimir Putin wa Urusi, Kirill Dmitriev, alielekea kwenye mikutano Januari 31 na wajumbe wa ujumbe wa Marekani katika jimbo la kusini la Florida. Pande hizo mbili zinaaminika kuratibu maoni yao kabla ya duru mpya.
Mazungumzo hayo ya pande tatu yanatarajiwa kuzingatia suala la eneo na uhakika wa usalama kwa Ukraine.