
Nyaraka hiyo mpya zimesababisha pia kujiuzulu kwa afisa wa ngazi ya juu nchini Slovakia na kufufua wito nchini Uingereza kwa aliyekuwa Mwanamfalme kushirikiana na wachunguzi wa Marekani.
Afisa huyo wa Slovakia, Miroslav Lajcak, amejiuzulu baada ya kufichuliwa kuwa alikutana na Epstein miaka kadhaa baada ya kuachiwa kutoka gerezani, ingawa hakutuhumiwa kufanya kosa lolote.
Aidha Waziri Mkuu wa Uingereza Keir Starmer amesema aliyekuwa mwanamfalme wa nchi hiyo na mtoto wa Malkia Elizabeth II aitwaye, Andrew anapaswa kutoa ushirikiano kamili kwa mamlaka za Marekani kuhusu uhusiano wake wa muda mrefu na Epstein.
Nyaraka hizo pia zinaonyesha mawasiliano ya Epstein na watu mashuhuri, wakiwemo aliyekuwa mshauri wa Rais Donald Trump, Steve Bannon, na wafanyabiashara maarufu kama Bill Gates na Elon Musk. Pia zinatoa mwanga juu ya uchunguzi uliosababisha mashtaka ya ulanguzi wa ngono dhidi ya Epstein mwaka 2019 na mshirika wake wa muda mrefu Ghislaine Maxwell mwaka 2021.