
Hiki ni kipindi kinachohusisha mahojiano ya kusisimua na wageni mbalimbali kutoka ndani na nje ya Japani. Wakati huu, tunakuletea Riwaya iitwayo “Tanaka-san Hataki Kwenda Ofisini” iliyoandikwa na Akeno Kaeruko
Mitindo ya kazi za ofisi imebadilika nchini Japani huku kufanyia kazi nyumbani kulikotokana na janga la virusi vya korona likiwa jambo la kawaida. Mhusika mkuu ni mwanaume mwenye umri wa makamo aliye na majivuno ambaye unaweza ukampata katika kampuni yoyote. Amekwamilia mno jinsi vitu vilivyokuwa vinafanywa na anahangaika kufanya kazi kwa kutumia mitindo mipya. Simulizi hii inaonyesha hali yake ya huzuni kwa kutumia ucheshi kiasi.
Mwandishi Akeno Kaeruko amebobea katika simulizi zinazohusu kazi, akitumia tajiriba zake za kazi ya ofisi.
Aidha, utasikiliza namna watangazaji wetu wanavyozamia gumzo za kuvutia zitakazokuacha ukivunjika mbavu. Hatimaye, kipindi kitafikia ukingoni baada ya sisi kutangamana nawe msikilizaji kwa kusoma ujumbe wako. Usikose kusikiliza
Kipindi hiki kilitangazwa Juni 23.