Hiki ni kipindi kinachohusisha mahojiano ya kusisimua na wageni mbalimbali kutoka ndani na nje ya Japani na mambo mengine ya kufurahisha.
Wakati huu, tunakuletea riwaya inayoitwa “Uvumi Kuhusu Bwana Aoyama” iliyoandikwa na Kodama.

“Uvumi Kuhusu Bwana Aoyama” ni insha ya kukonga nyoyo kuhusu mwalimu wa sanaa wa shule ya sekondari ya chini. Bwana Aoyama hana mvuto wa mwonekano, lakini kwa sababu fulani alikuwa maarufu kwa wanafunzi wake. Uvumi fulani kuhusu Bwana Aoyama ulisambazwa kwa mamlaka makubwa, na ulitumika kuimarisha taswira yake tu kama mwalimu.
Kodama, mwandishi, amewahi kufanya kazi kama mwalimu. Insha zake nyingi za kimashairi ni za kugusa kihisia na za kufurahisha. Kazi zake kuhusu familia na mtaa aliokulia na uzoefu wake wa maisha zinaendana na kumbukumbu ambazo kila mtu anazo. Pata ladha ya hisia hiyo murua kwa kufuatilia simulizi hii kuhusu kumbukumbu zake za shule ya sekondari ya chini.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *