Ujerumani yakemea Iran kutaja jeshi la EU kama magaidiUjerumani yakemea Iran kutaja jeshi la EU kama magaidi

Hatua iliyofuata baada ya Umoja Ulaya kuweka Kikosi cha Walinzi wa Mapinduzi cha Kiislamu cha Iran (IRGC) kwenye orodha ya makundi ya kigaidi.

Wadephul ameitaja hatua ya Iran kuwa haina msingi na ni propaganda, akisisitiza kuwa Ujerumani haitatishwa katika msimamo wake.

Kauli hiyo imetolewa baada ya Spika wa Bunge la Iran, Mohammad Bagher Ghalibaf, kutangaza kwamba majeshi ya Umoja wa Ulaya sasa yanachukuliwa kuwa makundi ya kigaidi, hatua iliyoungwa mkono na wabunge waliovaa sare za IRGC na kuimba kauli kali dhidi ya Marekani na Israel.

Wadephul amesema hatua ya Iran haibadilishi ukweli kuwa IRGC ni kikundi cha kigaidi, na kwamba wale wanaosambaza hofu na ukatili dhidi ya waandamanaji wa amani hawawezi kugeuza maoni ya kimataifa kwa njia za kisiasa. IRGC ni kikosi cha kipekee cha jeshi la Iran, kikiwa na ushawishi mkubwa kisiasa, kijamii na kiuchumi, na kimeendelea kupanua uwezo hata kupitia biashara na uwekezaji.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *