
Kupitia mtandao wa kijamii wa X, Zelenskiy amesema katika kipindi cha wiki moja pekee, Urusi imetumia zaidi ya droni 980, takribani mabomu 1,100 na makombora mawili dhidi ya Ukraine, akisisitiza umuhimu wa kuimarisha ulinzi wa anga.
Huku haya yakijiri Katibu wa Baraza la Ulinzi wa Taifa nchini Urusi, Sergei Shoigu, amewasili China kwa mazungumzo na Waziri wa Mambo ya Nje Wang Yi kuhusu masuala ya usalama wa kimataifa na kikanda.
Ziara hiyo inafanyika sambamba na mazungumzo ya hivi karibuni kati ya Urusi, Ukraine na maafisa wa Marekani yanayolenga kutafuta njia ya kumaliza vita vinavyoendelea kwa karibu miaka minne.