AGRICOM WAJIPANGA KUFANYA KAZI NA WAKULIMA KUBORESHA KILIMO ENDELEVU
Kongamano kubwa la kilimo Endelevu limeanza leo jijini Dar es salaam na wadau wa Kilimo wanatumia Fursa hiyo kueleza namna wamejipanga kufanya kazi na wakulima wa hapa nchini na nje ya mipaka yake.
Kutoka Agricom Afisa Masoko na Mauzo ndugu Mkali Crispo anasema wamedhamiria kushirikiana na wakulima na kufanya maajabu kwenye Kilimo endelevu.