Abiy Ahmed amesema hayo kwenye hotuba yake mbele ya bunge leo Jumanne na kuongeza kuwa licha ya mauaji hayo kwenye mji wa Axum, Eritrea pia ilifanya uporaji katika eneo la Adwa.

Waziri wa Mawasiliano wa Eritrea Yemane Gebremeskel hata hivyo hakutaka kuzungumzia madai hayo, alipoulizwa na shirika la habari la AFP.

Rais wa Eritrea Isaias Afwerki mnamo Februari 2023, alikana madai ya ukiukwaji wa haki za binaadamu huko Tigray na kuyataja kama ni ya uongo.

Uhusiano baina ya Ethiopia na Eritrea umezidi kuzorota tangu walipopigana pamoja dhidi ya waasi wa Tigray, na hii ni mara ya kwanza kwa Abiy kukiri mauaji hayo yaliyofanywa na Eritrea.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *