Makubaliano hayo yaliyofikiwa usiku wa Jumatatu (Februari 2) yalikuja wakati Mwenyekiti wa Kamati ya Uchunguzi ya Bunge, James Comer, akitayarisha hati ya mashitaka ya uhalifu dhidi ya wawili hao, kwa kukaidi kwao wito wa bunge.

Mawakili wa Clinton waliiarifu Kamati hiyo kupitia barua-pepe kwamba wateja wao walikuwa tayari kufikia makubaliano juu ya tarehe za kutoa ushahidi.

Hii itakuwa mara ya kwanza kwa Kamati hiyo kumuita rais wa zamani kwenye uchunguzi, ambao kama ukimtia hatiani, unaweza kuwa kesi yenye kifungo gerezani.

Clinton alikuwa na uhusiano mkubwa na Epstein katika miaka ya 1990 na 2000, licha ya kwamba hajawahi kushitakiwa kwa kosa lolote kwenye mahusiano hayo. 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *