
Msemaji wa Ikulu ya Urusi, Dmity Peskov amesema pendekezo la Rais Vladmir Putin bado liko mezani, lakini Marekani bado haijajibu, na ameonya kuwa katika siku chache zijazo, dunia itakuwa katika hali ya hatari zaidi kuliko ilivyokuwa.
Mikataba ya awali ya New START iliyosainiwa kati ya Marekani na Jamhuri ya Kisovieti, iliainisha upunguzaji wa makombora ya nyuklia na vichwa vyake.
Lakini mkataba uliosainiwa mwaka 2010, unaweka ukomo wa vichwa 1,550 vya nyuklia kwa kila upande, na mifumo 800 ya kusafirisha vichwa hivyo.
Mwaka mmoja baada ya kuanza kwa vita vya Ukraine, Rais Putin alisitisha ushiriki wa Urusi katika mkataba wa New START mwaka 2023, akitoa sababu kwamba wakaguzi wa Urusi walikuwa hawawezi tena kuzuru vituo vya silaha vya Marekani.