Kutokana na kuongezeka kwa matukio ya ubadhirifu, migogoro na usimamizi usioridhisha katika baadhi ya taasisi za kidini, vyama vya michezo na asasi za kiraia, Wakala wa Usajili Ufilisi na Udhamini (RITA imeandaa mafunzo maalum kwa wajumbe wa Bodi za Wadhamini katika mikoa sita.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dodoma, Kabidhi Wasii Mkuu na Afisa Mtendaji Mkuu wa RITA, Frank Kanyusi Frank, amesema washiriki watapata mafunzo ya matumizi ya mfumo wa kielektroniki wa eRITA unaotumika katika usimamizi na uwasilishaji wa taarifa kwa njia salama na ya haraka.
“Mafunzo hayo yatafanyika kwa siku mbili kuanzia Februari 11 mkoani Katavi na kuhusisha washiriki 500 kutoka mikoa ya Kigoma, Tabora, Rukwa, Mbeya na Songwe,” amesema Kanyus.
Kwa mujibu wa Kabidhi Wasii Mkuu, mafunzo hayo yanalenga kuwajengea uwezo katika kutekeleza majukumu yao wakizingatia sheria, kanuni, taratibu na kusimamia katiba za taasisi zao ambako Waziri wa Katiba na Sheria, Dkt Juma Homera atafungua.
#StarTvUpdate