Uamuzi huo unatolewa katikati ya maandamano yaliyosambaa pamoja ukosoaji baada ya kisa cha raia wa Marekani kuuliwa na maafisa wa uhamiaji katika mji huo wa Minneapolis

Rais Donald Trump, ambaye alibatilisha agizo kama hilo lililotolewa na mtangulizi wake Joe Biden ameonekana kuunga mkono uamuzi wa Noem alipozungumza na waandishi wa habari ofisini kwake mjini Washington.

Amesema “Haikuwa uamuzi wangu. Ningemwachia, unajua, hilo. Kwa ujumla camrea huwa ni kwa watekezaji wa sheria kwa sababu hawawezi kudanganya kuhusu kinachoendelea. Kwa hivyo, kwa ujumla, nadhani kwa asilimia 80 ni hatua nzuri kwa vyombo vya sheria. Na ikiwa anataka kufanya hivyo, nakubaliana nalo. Kumbuka jambo moja, tulifunga mpaka. Nilichaguliwa wakati kuna hali mbaya mpakani, lakini sasa hakuna anayeingia kupitia mpaka wetu tena.”

Noem ameahidi uamuzi huo kutekelezwa kote nchini humo baada ya fedha kupatikana.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *