Tom Félix, Mfaransa aliyekuwa anakabiliwa na adhabu ya kifo nchini Malaysia kwa kumiliki na kufanya biashara ya dawa za kulevya—mashtaka ambayo alikanusha mara kwa mara—amefutiwa mashitaka leo Jumanne, Februari 3, 2026. Ataachiliwa huru baada ya zaidi ya siku 900 kizuizini.

Imechapishwa:

Dakika 2 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Afisa huyo wa zamani wa kampuni ya Ufaransa ya Veolia, mhitimu wa kilimo cha samaki na biolojia ya baharini, alikuwa karibu kufungua mgahawa huko Langkawi alipokamatwa mnamo Agosti 9, 2023, katika kisiwa hiki kaskazini magharibi mwa Malaysia. Katika nyumba aliyokuwa akiishi na mshirika wake wa biashara wa Malaysia, polisi walipata kilo 1.86 za bangi katika maeneo ya kawaida. Wanaume wote wawili walikamatwa. Familia yake ilisisitiza kwamba, wakati wa uchunguzi, Tom Félix aliondolewa mashtaka na mshirika wake wa biashara.

“Mwisho wa jinamizi”

“Katika kesi hii, mahakama ilishindwa kuthibitisha ushahidi wa hatia, (…) mshtakiwa amefutiwa mashitaka na kuachiliwa huru,” Jaji Evawani Farisyta Mohammad wa Mahakama Kuu ya Jinai ya Alor Setar, jiji lililoko kilomita 500 kaskazini magharibi mwa Kuala Lumpur, ambapo kijana huyo Mfaransa, mwenye umri wa miaka 34 alikuwa akishikiliwa. Tom Félix anatarajiwa kuachiliwa ndani ya saa chache zijazo baada ya kukamilisha taratibu mbalimbali.

“Huu ni mwisho wa jinamizi, na tunafurahi sana,” Sylvie Félix, mama yake Tom, amejibu akihojiwa na shirika la habari la Agence France-Presse alipotoka mahakamani. “Tunashukuru sana kwa msaada wa familia yetu yote, na sasa kwa kuwa yeye (Tom) ameachiliwa huru, tunafanya kila tuwezalo kuhakikisha anarudi (Ufaransa) salama na haraka iwezekanavyo.”

Rais Emmanuel Macron, ambaye alikutana na wazazi wote wawili mnamo mwezi Mei 2025 wakati wa ziara ya serikali nchini Singapore, ambapo wanafundisha katika shule ya Ufaransa, alielezea “furaha yake kubwa” katika ujumbe kwenye mtandao wa kijamii wa X. “Nafikiria wazazi wake, ambao nilikutana nao, ambao hawakuacha kuamini na ambao sasa wataungana tena na mwanao,” rais wa Ufaransa ameongeza.

Kesi ndefu za kisheria

Baada ya kikao cha awali cha Januari 14, ambapo mwendesha mashtaka aliwasilisha hoja zake, Mfaransa huyo kijana, akionekana mwembamba, alijitokeza tena siku ya Jumanne alasiri. Wazazi wake, Sylvie na Jean-Luc Félix, ambao wamehudhuria kila kikao cha mahakama, walikuwepo tena mahakamani leo Jumanne.

Kulingana na wakili wake kutoka Malaysia, Collin Andrew, kulikuwa na matokeo mawili yanayowezekana: “Mahakama inaweza kugundua kuwa upande wa mashtaka umeshindwa kuthibitisha hatia yake, ambapo Tom Félix atafutia mashitaka na kuachiliwa huru.” “Lakini mahakama inaweza pia kuamua kuendelea na kesi na kisha kuita utetezi kuwasilisha hoja zake baadaye, kabla ya uamuzi wa mwisho,” wakili huyo ameongeza. Baada ya mchakato mrefu wa kisheria na kipindi kigumu sana cha kuzuiliwa kwa Tom Félix, chini ya mazingira ngumu, jaji ameamua Jumanne kwamba ushahidi wa hatia yake haukuwa umethibitishwa.

Ikiwa angepatikana na hatia, kijana huyo Mfaransa angekabiliwa na adhabu ya kifo au kifungo cha jumla cha miaka 104 jela, viboko 54, na faini ya euro 27,000.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *