
Waziri anayehusika na Ujenzi Mpya Oleksiy Kuleba amesema kupitia mitandao ya kijamii kwamba Urusi imeshambulia makazi, miundombinu ya kusambaza joto na kuvuruga malazi ya watu kote nchini humo.
Mkuu wa utawala wa kijeshi wa Kyiv Tymur Tkachenko ameandika kupitia mtandao wa Telegram, akiwaomba wakazi kubakia ndani na baadae alisema watu wawili walijeruhiwa.
Haya yanajitokeza wakati, awamu ya pili ya mazungumzo ya utatu kati ya Ukraine, Marekani na Urusi yakitarajiwa kufanyika Umoja wa Falme za Kiarabu siku ya Jumatano na Alhamisi, hii ikiwa ni kulingana na msemaji wa Kremlin, Dmitry Peskov.