Mbunge mstaafu, Munde Tambwe amefariki dunia baada ya kuugua kwa mrefu.
Tambwe ambaye alikuwa mbunge wa viti maalum kupitia Mkoa wa Tabora katika Bunge lililopita chini ya Spika Dkt Tulia Ackson amefariki dunia usiku wa kuamkia leo katika hospitali ya Taifa Muhimbili.
Hata hivyo, katika kinyang’anyiro cha kuwania kurejea bungeni mwaka 2025 mbunge huyo aliangukia pua baada ya jina lake kukatwa na Kamati Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), licha ya kushinda kura za maoni katika Jimbo la Sikonge, Tabora.
Mbunge wa Mtama (CCM), Nape Nnauye kupitia ukurasa wake wa Instagram amemlilia mbunge huyo na kusema kuwa wema, upendo na ukweli wake hatovisahau daima.
#StarTvUpdate