Mshauri mwelekezi wa masuala ya elimu kutoka shirika la HakiElimu, Dkt. Wilberforce Meena, amesema moja ya sababu zinazochangia wanafunzi wa awali na msingi kuchelewa kujua kusoma, kuandika na kuhesabu ni uwepo wa idadi kubwa ya wanafunzi katika darasa moja.
Amesema hali hiyo humnyima mwalimu nafasi ya kufuatilia na kukagua maendeleo ya kila mwanafunzi mmoja mmoja, jambo linalosababisha kushindwa kubaini mapema changamoto zinazowakabili na kutoa msaada unaohitajika.
✍Halima Addallah
Mhariri | John Mbalamwezi
#AzamTVUpdates