Ofisi ya Uhamiaji Mkoa wa Morogoro imewakamata raia 14 wa kigeni kutoka mataifa ya Burundi na Ethiopia kwa tuhuma za kuingia na kuwepo nchini bila vibali halali.
Akizungumza na waandishi wa habari, Kamishna Msaidizi wa Uhamiaji mkoa wa Morogoro, Sada Natepe amesema watuhumiwa hao wanatarajiwa kufikishwa mahakamani baada ya taratibu za upelelezi kukamilika.
#AzamTVUpdates
Mhariri | John Mbalamwezi