Msemaji wa wizara ya Mambo ya Nje ya Qatar, Majed al-Ansar amewaambia wandishi wa habari kuwa juhudi zinaendelea kwa nguvu kubwa kwa wakati huu na Qatar imekuwa ikishirikiana na majirani zao wakiwemo Misri, Oman, Saudi Arabia na Uturuki.

Amesema “Hii imekuwa inatokea katika katika siku chache zilizopita, siyo na Qatar, lakini pia na pande zote za kikanda. Bila shaka kuna mawasiliano ya ngazi ya juu, kama ambavyo mmeona, yanayolenga kupunguza mzozo katika kanda na kuzuwia kurudi kwenye uchochezi.”

Rais wa Iran Masoud Pezeshkian alisema Jumanne kuwa amemuagiza waziri wa mambo ya nje kuanzisha majadiliano ya haki na usawa na Marekani katika ishara ya kwanza kutoka Tehran kwamba inataka kujaribu kufanya majadiliano wakati mzozo ukipamba moto na Washington, kufuatia ukandamizaji mkali kwenye maandamano ya kitaifa mwezi uliopita.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *