
Pezeshkian amesema kupitia mtandao wa X kwamba amemuagiza Araghchi kufanya mazungumzo hayo kwa kuongozwa na misingi ya utu, busara, na uthabiti, lakini kwa kuzingatia mazingira yanayofaa, yasiyokuwa na vitisho na matarajio yasiyo na msingi.
Aidha ameagiza kwamba mazungumzo hayo “yafanyike ndani ya mfumo wa maslahi ya taifa hilo.”
Kulingana na vyombo vya habari vya Marekani, Araghchi anatarajiwa kufanya mazungumzo ya nyuklia na mjumbe maalumu wa Marekani Steve Witkoff mjini Istanbul siku ya Ijumaa.
Hata hivyo Wairan wengi wanapinga vikali makubaliano na Marekani, wakihisi kama wamesalitiwa na Rais Donald Trump aliyeahidi kuwasaidia waandamanaji wanaoipinga mamlaka nchini humo.