Serikali imesema inaendelea kufanya maboresho katika Bandari ya Dar es Salaam, ikiwemo kujenga gati namba 12 hadi 15 ili kuongeza ufanisi na uwezo wa bandari hiyo kuhudumia meli nyingi.

Hayo yamesemwa hii leo bungeni Dodoma na Naibu Waziri wa Uchukuzi, David Kihenzile, wakati akijibu swali la Mbunge wa Bumbwini, Mwinyi Jamal Ramadhan aliyehoji juu ya bandari kushindwa kupokea meli nyingi kwa wakati mmoja.

#AzamTVUpdates
Mhariri | John Mbalamwezi

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *