Serikali kupitia wizara ya elimu imefanya uzinduzi wa mkakati wa kisayansi wa kujenga umahiri katika kusoma, kuandika na kuhesabu kwa madarasa ya awali, hii ni kutokana na kuwepo kwa wimbi kubwa la wanafunzi wa awali na shule ya msingi kuchelewa ama kutokujua kabisa kusoma ,kuandika na kuhesabu .

Mdau wa Elimu, Justine Kakoko amesema uwepo wa mfumo wa KKK utasaidia wanafunzi wa awali na wa shule ya msingi kuelewa kwa haraka kusoma na kuandika.

Ameeleza kuwa ujuzi wa hatua za awali yaani KKK ni muhimu kwa watoto wa awali kwasababu akikosa ujuzi huo atapata ugumu wa kujifunza katika hatua za mbeleni.

✍Halima Addallah
Mhariri | John Mbalamwezi

#AzamTVUpdates

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *