Idara ya Kukabiliana na Moto na Majanga ya Japani inasema hali mbaya za majira ya baridi kali na ajali zinazohusiana na theluji katika siku 14 zilizopita, zimesababisha vifo vya watu 27.
Kufikia Februari 2, watu 12 walikuwa wamekufa katika mkoa wa Niigata kwenye pwani ya Bahari ya Japani, sita katika mkoa wa Akita, kaskazini mwa Japani, na watatu katika mkoa wa kaskazini kabisa wa Hokkaido. Vifo viwili vilitokea Aomori, kaskazini mwa Japani. Mikoa ya Iwate, Yamagata, Nagano, na Shimane kila moja uliripoti kifo kimoja.
Maafisa wa mkoa wa Niigata wanasema wanaume wawili waliokuwa wakiondoa theluji Februari mosi walisombwa katika njia ya maji ya kuondolea theluji. Wengine walionekana kuanguka kutoka kwenye paa au kufariki baada ya kuugua ghafla kazini au wakati wa mapumziko.
Jumla ya watu 290 walipata majeraha, baadhi makubwa, kutokana na matukio yanayohusiana na theluji.