Umoja wa Mataifa unatarajiwa kutuma ujumbe wake huko Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo kufanikisha usitishwaji wa mapigano.
Uamuzi huo unakuja siku moja baada ya kikao kilichofanyika Doha, kilichohusisha wawakilishi wa kikosi cha waasi cha M23 na wajumbe kutoka DRC.
“Wakati wa kikao hicho, pande zote mbili zilikubaliana kuwepo na mfumo maalumu wa ufatiliaji wa kukomesha mapigano”, ilisomeka sehemu ya taarifa iliyotolewa na serikali ya Qatar.
Mwezi Januari mwaka jana, kikundi cha M23 kilidhibiti mji wa Goma, kabla ya kushikilia mji wa Bukavu, mwezi uliofuata.