Wakaazi katika vijiji vya Ukingo wa Magharibi wafurushwaWakaazi katika vijiji vya Ukingo wa Magharibi wafurushwa

Jamila Rashid na familia yake wameishi kwenye kijiji cha Ras Ein el-Auja cha wapalestina wa jamii ya waBedoui kusini mwa bonde la Jordan. Hata hivyo alilazimika kuondoka mwanzoni mwa Januari hii. Ameelezea kuwa walowezi wa Kiyahudi wamewahangaisha sana,kwenye maeneo yao katikati mwa Ukingo wa Magharibi.

Mama huyo ameilezea DW kwamb hakuna tena usalama na kwamba wametaabika kwa miaka mitatu lakini kwa sasa uhasama umezidi. Amesema alivamiwa jikoni kwake na watoto walitishika mno.

Katika kipindi cha mwaka mmoja uliopita, matukio ya uhasama na vurugu yanayofanywa na walowezi wa Kiyahudi kuwalenga waPalestina yameongezeka katika Ukingo wa Magharibi.Uvamizi umeongezeka tangu mashambulizi ya Hamas ya Oktoba 2023 nchini Israel na vita vya Gaza kwa jumla.

Takwimu za jeshi la Israel IDF na shirika la usalama wa taifa la Shin Bet, zinaonyesha kuwa idadi ya mashambulizi ya walowezi walio na msimamo mkali dhidi ya waPalestina na pia ya vikosi rasmi yameongezeka kwa asilimia 27 katika mwaka wa 2025 ikilinganishwa na mwaka uliotangulia wa 2024.

Kwa upande wake afisi ya Umoja wa Mataifa ya kuratibu misaada ya kibinadamu,OCHA, zaidi ya familia 700 za waPalestina zimejikuta bila makaazi kwasababu ya uvamizi na uhasama wa walowezi wa Kiyahudi kwenye eneo la Ukingo wa Magharibi. Baadhi ya walioathirika ni jamii za waBedoui na wafugaji kwenye eneo la Area C ambalo ndilo kubwa zaidi kwenye Ukingo wa Magharibi unaosimamiwa kikamilifu na serikali ya Israel. Kwa mujibu wa shirika la kutetea haki za binadamu la Israel B’Tselem ,jamii zipatazo 44 zimefurushwa tangu Oktoba 2023.

Hali katika kijijni cha Ras Ein el-Auja ilianza kuvurugika mwishoni mwa Disemba mwaka uliopita pale walowezi wa Kiyahudi walipotenga kituo haram ndani ya kijiji hicho. Walilima ardhi hiyo kwa matrekta na kuifunga barabara iliyoelekea upande mmoja wa jamii hiyo.

Palestina Gebiete Qalandya 2026 | Polisi ya Israeli
Maafisa wa polisi wa Israel wakishika doria kijiji cha Qalandya, Ukingo wa MagharibiPicha: Mohamad Torokman/REUTERS

Salameh Qa’abna mkaazi wa eneo hilo anasema walizuiliwa kutumia barabara hiyo na kuyafikia matangi ya maji.Walikja hadi karibu na sehemu zetu za kulala. Tulijawa na hofu. Takwimu zinaashiria kuwa watu wapatao 130 kutokea familia mbalimbali za Wabedoui wamelazimika kuvunja nyumba zao na kuondoka kijijini hapo mapema mwezi huu kwasababu ya uhasama na uvamizi.

Kinachotokea Ras Ein el-Auja ambacho ni kijiji kilichozingirwa na majengo kadhaa haramu sio cha ajabu. Hali hiyo imejirudia kwenye jamii nyingi tofauti za Wapalestina mfano Muarrajat na Mughayyir al-Deir. Huko pia walowezi walijenga vituo haramu katikati ya vijiji, wameongeza uvamizi na kuwafurusha wakaazi katika kipindi kifupi.

Kulingana na watetezi wanaopinga ulowezi, Peace Now, makaazi zaidi ya 149 yanapatikana kote Ukingo wa Magharibi vikiwemo vyengine 224 ambavyo ni vituo haramu pamoja na mashamba. Ifahamike kuwa vituo hivyo vinakiuka sheria za kimataifa ila Israel inalipinga hilo. Kila serikali ambayo imekuwa madarakani Israel imekuwa ikisogeza mbele hoja ya kupanua makazi ya walowezi tangu ilipoudhibiti Ukingo wa Magharibi katika vita vya mwaka 1967,.

Wapalestina waanza kuhama kuelekea kusini mwa Gaza

To view this video please enable JavaScript, and consider upgrading to a web browser that supports HTML5 video

Kwa sasa serikali ya Israel imetangaza kuwa imehalalisha ujenzi wa makaazi mapya 19 pamoja na kutekeleza mpango unazoua hisia mseto wa E1 utakaougawa Ukingo wa Magharibi mara mbili. Hatua hii inatazamwa kama kikwazo katika mchakato mzima wa kusaka amani ya kudumu na kuunda dola la Palestina.

Kwa upande wake, jeshi la Israel, IDF, katika taarifa yake linasisitiza kuwa limeiongeza idadi ya wanajeshi wake wanaopiga doria na kwamba linafahamu kinachoendelea. IDF inabainisha kuwa vikosi vyake vinaingia kwenye eneo hilo kuzuia mivutano na uhasama na kuingilia kati ikihitajika.

Kijijini Ras Ein el-Auja, Rashid,Qa’abna na jamaa zao wamamua kuondoka na kuzisafirisha jamii zao hadi kwenye maeneo salama. Wafugaji nao pia waliondoka na wanyama wao. Kilichosalia ni vibanda tu, ishara kuwa jamii ziliishi hapo kwa miaka kadhaa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *