
Kurejea kwao kulitanguliwa na kuwasili kwa kundi dogo la waokoaji kutokea Ukanda huo kuingia upande wa Misri jioni ya Jumatatu (Februari 2).
Kufunguliwa tena kwa kivuuko hicho ni sehemu muhimu kwenye kile kiitwacho makubaliano ya kusitisha mapigano kati ya Israel na wanamgambo wa Kipalestina, ambayo hata hivyo yamekuwa yakivunjwa mara kadhaa, tangu yalipotangazwa mwezi Oktoba.
Siku ya Jumatatu, Mtoto wa Kipalestina mwenye umri wa miaka mitatu aliuawa kwa mashambulizi ya jeshi la Israel dhidi ya kambi ya wakimbizi huko Khan Younis.
Wapalestina wengine wanne waliuawa na Israel kaskazini mwa Gaza, kwa madai ya kupita eneo lililohatarisha usalama wa jeshi lake.
Kwa mujibu wa mamlaka za afya za Gaza, zaidi ya Wapalestina 520 wameshauwa tangu yalipotangazwa makubaliano ya kusitisha mapigano mnamo Oktoba 10, na hivyo kuifanya idadi ya Wapalestina waliokwisha kuuawa tangu Oktoba 2023 kufikia 71,800.