Waziri Mkuu wa Ethiopia, Abiy Ahmed, jana alieleza kuwa Chuo Kikuu cha pili duniani kilichojikita katika akili mnemba (AI) kinatarajiwa kuzinduliwa nchini Ethiopia mwaka kesho wa 2027.

Tovuti ya habari ya Standard yenye makao yake huko Addis Ababa imeripoti kuwa Waziri Mkuu wa Ethiopia ameliambia Bunge kwamba ujenzi wa chuo hicho unaendelea, na kinatarajiwa kuanza shughuli zake mwakani.

Abiy Ahmed amesisitiza umuhimu wa kuandaa vijana wa Ethiopia kwa changamoto za siku zijazo na kuongeza kuwa teknolojia ni “mojawapo ya nguzo tano za maendeleo ya Ethiopia.”

“Kama ambavyo mababu zetu walianzisha Shirika la Ndege la Ethiopia na kulifanya kuwa taasisi inayoheshimika duniani kote, chuo hicho kikuu pia kitafungua zama bora na za juu zaidi kwa watoto wetu,” amesema Waziri Mkuu wa Ethiopia.

Hata hivyo Bunge la Ethiopia halikuweza wazi muundo wa chuo hicho kikuu, mitaala au mfumo wake wa fedha.

Mwezi Januari mwaka huu Abiy Ahmed alitangaza mipango ya kutoa mafunzo ya akili mnemba katika chuo hicho ambacho kitajikita pakubwa katika nyanja kama vile kujifunza kwa kutumia mashine, roboti, sayansi ya data n.k.

 Amesisitiza kuwa chuo hicho  kitatoa nafasi 100 za ufadhili wa masomo huku nafasi 2 zikiwekwa kando kwa ajili ya wanafunzi kutoka kila nchi ya Afrika Mashariki. 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *