Rais wa Mahakama Kuu ya Kijeshi, Maria Elizabeth Rocha, amesema mahakama hiyo itajadili ombi lililowasilishwa na waendesha mashitaka kumtangaza Bolsonaro na makamanda wengine wa ngazi za juu kutokuwa na haki ya kubakia na vyeo vyao na mafao kutoka jeshini.

Hii ni mara ya kwanza kwa mahakama hiyo kuanzisha mchakato wa kumvua cheo jenerali wa kijeshi.

Bolsonaro, mwanajeshi wa zamani aliyekuwa na cheo cha kapteni, alihukumiwa kifungo cha miaka 27 jela na Mahakama ya Juu mnamo mwezi Septemba, baada ya kukutwa na hatia ya kupanga njama za kusalia madarakani kufuatia kushindwa kwake na rais wa sasa, Luiz Inacio Lula da Silva, kwenye uchaguzi wa mwaka 2022. 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *