Chama cha Wasambazaji wa Bidhaa na Watoa Huduma Migodini (TAMISA), kimewataka vijana kuchangamkia mikopo inayotolewa na Serikali kwa ajili ya kuwawezesha kupata mitaji.
Mwenyekiti wa TAMISA, Peter Kumalilwa amesena katika jitihada za kuongeza ajira na kukuza uchumi kupitia sekta ya madini, Serikali imetenga kiasi cha Sh5 trilioni kwa ajili ya kuwawezesha Watanzania wanaojihusisha na shughuli za usambazaji wa bidhaa na utoaji wa huduma katika migodi mbalimbali nchini.
“Vijana watapewa kipaumbele katika utoaji wa huduma hizi migodini, hivyo tunawaomba wajitokeze kwa wingi kuchangamkia fursa hizi.”
Kwa upande wake, Afisa Mtendaji Mkuu wa TAMISA, Japhet Mussa, amesema Serikali inatambua dhamira ya Watanzania wengi ya kushiriki katika biashara ya madini na iko tayari kuunga mkono jitihada hizo ili kuongeza ushiriki wa wazawa katika mnyororo wa thamani wa sekta hiyo.
#starTvUpdate