Jeshi la Sudan limesema limeuvunja mzingiro wa miaka mingi katika mji wa Kadugli na kutoa matumaini kwa maelfu ya watu wanaokabaliwa na kitisho cha baa la njaa, na kuashiria mabadiliko katika mwelekeo wa vita vinavyoikumba nchi hiyo.

Miji ya Kadugli na mji jirani wa al-Dalanj ilikuwa imezingirwa tangu kuanza kwa vita nchini Sudan kati ya majeshi ya serikali na vikosi vya RSF.

Umoja wa Mataifa umesema mzingiro huo uliowekwa na wapiganaji wa RSF ulisababisha mji wa Kadugli kukaribia kutumbukia kwenye baa la njaa. Jan Egeland ni mkuu wa Baraza la wakimbizi la Norway amesema kuwa ameshtushwa na kile alichokiona, akielezea kuwa ni mateso makubwa, yasiyodhibitiwa na jumuiya ya kimataifa kutojihusisha kikamilifu katika kuishughulikia hali hii, ambako ndio eneo kubwa na baya zaidi la mgogoro, na pia ndiyo janga kubwa zaidi la njaa.

Takriban watu 147,000 ambao ni asilimia 80 ya idadi ya watu wa Kadugli walilazimika kuukimbia mji huo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *