Kampuni kubwa zaidi ya kuzalisha umeme ya Japani ya Jera, imetia saini mkataba wa muda mrefu wa kununua gesi asilia ya kimiminika, LNG kutoka Qatar, kuanzia mwaka 2028. Jera inasema makubaliano hayo yanatoa chanzo thabiti cha fueli ili kukidhi ongezeko la mahitaji ya umeme.

Februari 3, Jera ilisema itanunua tani takribani milioni 3 za LNG kwa mwaka kutoka QatarEnergy inayoendeshwa na serikali kwa miaka 27. Kiwango hicho ni karibu asilimia 5 ya matumizi ya LNG ya kila mwaka ya Japani. Jera haikutoa bei ya ununuzi.

LNG ni fueli muhimu kwa mitambo ya umeme wa joto. Bei yake ilipanda miaka minne iliyopita wakati uvamizi wa Urusi dhidi ya Ukraine ulipovuruga njia za usambazaji wa umeme duniani.

Sasa, usambazaji thabiti wa LNG umechukua umuhimu mpya kwani matumizi ya akili unde zalishi yanaongeza mahitaji ya umeme katika vituo vya data.

Mkataba wa Jera na Qatar sio wa kwanza. Ilikuwa na mkataba uliodumu hadi 2021 wa kununua tani zaidi ya milioni 6 za LNG kwa mwaka kutoka nchini humo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *