
Mwakilishi wa Biashara wa Marekani, Jamieson Greer, amesema ofisi yake sasa itashirikiana na Baraza la Congress mwaka huu ili kuifanya programu hiyo kutowa fursa zaidi za soko kwa ajili ya bidhaa, wakulima na wawindaji wa Marekani, ili kuendana na sera ya Marekani Kwanza ya Rais Trump.
Programu hiyo iitwayo kwa kifupi AGOA ilianzishwa kwa mara ya kwanza mwaka 2000 ili kutowa fursa ya soko lisilo ushuru kwa bidhaa za mataifa ya Afrika Kusini mwa Jangwa la Sahara.
Ilifikia mwisho wake mnamo Septemba mwaka jana na kuhatarisha usalama wa nafasi za ajira kwa mamia kwa maelfu ya Waafrika.
Licha ya mwezi uliopita, Baraza la Wawakilishi kupiga kura ya kuiongezea muda wa miaka mitatu, Baraza la Seneti iliupunguza hadi kuwa mwaka mmoja tu, unaoishia mwishoni mwa mwaka huu.