Dadake Saif al-Islam Gaddafi aliviambia vyombo vya habari vya Libya kuwa alifariki karibu na mpaka wa Libya na Algeria

Chanzo cha picha, Reuters

Muda wa kusoma: Dakika 4

Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali ilithibitisha kuwa maafusa wa polisi wanalilinda eneo la tukio na kwa ajili ya kuanza taratibu rasmi muda mfupi baada ya mwili wake kupatikana.

Mamlaka bado haijafichua makabiliano ya risasi yalitokea wapi au ni nani aliyehusika. Hata hivyo walisisitiza tukio hilo linachukuliwa kuwa uhalifu wa jinai na kwamba taratibu zote zitafuatwa ili wahusika wachukuliwe hatua za kisheria.

Kifo chake kimetokea wakati ambapo Libya bado inakabiliwa na msukosuko unaotokana na makundi yenye silaha, mamlaka zinazopingana kisiasa, na utawala dhaifu wa serikali kuu unaendelea kuchochea ghasia.

Mamlaka Libya inasema nini?

The Attorney General’s Office confirmed that law enforcement teams secured the scene and began formal procedures shortly after the body was found. Officials said forensic examinations were completed, and investigators are now focusing on reconstructing the events that led to his death.

Authorities have not yet disclosed where the shooting occurred or who may be responsible. However, they stressed that the case is being treated as a criminal matter and that all leads will be pursued to bring those responsible to justice.

The announcement comes amid ongoing instability in Libya, where armed groups, rival political authorities, and weak central governance continue to fuel violence and uncertainty.

Saif al-Islam Gaddafi ni nani?

Saif al-Islam Gaddafi, aliyezaliwa mwaka 1972, alionekana na baadhi ya watu kama mtu mwenye nguvu na ushawishi mkubwa zaidi nchini Libya baada ya baba yake.

Kwa miaka mingi, alitwishwa jukumu la umma utawala wa Gaddafi wa kufikia nchi za Magharibi, akijiweka kama mtu mwenye nia ya mageuzi huku akiwa bado na mamlaka makubwa.

Katika miaka ya mapema ya 2000, Saif al-Islam alikuwa kiungo muhimu katika kuhalalisha uhusiano wa Libya na mataifa ya Magharibi, kusaidia kufikiwa kwa mikataba ya ambayo ilisababisha kuondolewa kwa vikwazo na kurejea kwa Libya katika jumuiya ya kimataifa. Mara nyingi alijionyesha kama mtu wa kisasa, akikuza mageuzi ya kiuchumi na uwazi mdogo wa kisiasa.

Licha ya taswira hii, Walibya wengi walimwona kama mtekelezaji mkuu wa mamlaka ya serikali, haswa wakati wa maasi ya 2011 ambayo yalimaliza utawala wa miaka 42 wa baba yake.

Saif al-Islam aliyesomea nchini Uingereza alihudumu kama mwanadiplomasia asiye rasmi wa Tripoli, akishiriki katika mazungumzo yaliyopelekea Libya kuachana na mipango yake ya silaha za maangamizi makubwa mwanzoni mwa miaka ya 2000.

Lakini sifa yake iliharibiwa wakati wa maasi ya 2011, alipoapa kwamba Libya itageuka “mito ya damu” ikiwa maandamano dhidi ya utawala wa baba yake yataendelea.

Waasi wanaoungwa mkono na NATO walipokaribia kuangusha utawala wa baba yake, Seif alikua mmoja wa watetezi wa nguvu zaidi wa serikali. Baada ya kuporomoka kwa serikali, alikamatwa na wanamgambo wakati alipokuwa akujaribu kutoroka nchini, kulingana na ripoti.

Alizuiliwa kwa miaka sita huko Zintan, na mwaka 2015 na hatimaye hukumiwa kifo mahakama ya Tripoli – uamuzi ambao baadaye ulibatilishwa chini ya msamaha.

Saif al-Islam Gaddafi na maasi ya 2011 Libya

Maandamano yalipozuka nchini Libya mwaka 2011, Saif al-Islam aliibuka kuwa mmoja wa watetezi wakuu serikalini. Alitoa hotuba kali kuwaonya waandamanaji kuhusu machafuko na vita vya wenyewe kwa wenyewe, kauli ambazo baadaye ziligeuka kuwa mauaji ya kikatili ya utawala dhidi ya wapinzani.

Baada ya Muammar Gaddafi kuuawa Oktoba 2011 katika mji Sirte alikozaliwa, Saif al-Islam alitoweka macho pa watu kwa muda mrefu. Ushawishi wake ulididimia huku Libya ikisambaratika na kuwa serikali pinzani na wanamgambo.

Kesi zilizomuandama Saif al-Islam Gaddafi

Mnamo mwaka wa 2015, mahakama ya Libya ilitoa hukumu kifo dhidi ya Saif al-Islam ambaye hakuwepo mahakamani hapo, ikimtuhumu kwa uhalifu unaohusishwa na ukandamizaji wa maandamano wakati wa mapinduzi ya 2011.

Pia alishtakiwa katika Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu wa Jinai ICC, kwa tuhuma za uhalifu dhidi ya ubinadamu. Juhudi za mawakili wake kufuta kesi hiyo hazikufua dafu na hivyo kuacha mashtaka hayo bila kutatuliwa kwa miaka mingi.

Vita hivi vya kisheria vilimweka Seif al-Islam katika uangalizi wa kimataifa, licha ya kuishi maisha ya kutoonekana ndani ya Libya.

Mnamo 2021, Saif al-Islam alijaribu kurejea kisiasa kwa kujiandikisha kama mgombeaji wa urais kwa uchaguzi uliopangwa wa Libya. Kura iliporomoka kwa sababu ya mgawanyiko mkubwa wa kisiasa, na ombi lake lilishindwa kurejesha ushawishi wake wa zamani.

Wakati baadhi ya wafuasi wakiendelea kumwona kama mtu anayeweza kuwaunganisha, Walibya wengi walipinga kurejea kwake, wakitaja nafasi yake katika utawala wa zamani na tuhuma ambazo hazijatatuliwa dhidi yake.

Katika miaka ya hivi karibuni, uwepo wake hadharani ulipungua zaidi, na kufanya habari za kifo chake kuwa zisizotarajiwa zaidi.

Mnamo 2021, Saif al-Islam alijaribu kurejea katika ulingo wa kisiasa kwa kujiandikisha kuwa mgombea urais katika uchaguzi uliopangwa wa Libya. Hata hiyo azma yake ya kurejesha ushawishi wake wa zamani haikutimia kutokana na mgawanyiko mkubwa wa kisiasa ulioibuka.

Wakati baadhi ya wafuasi wakiendelea kumuwona kama mtu anayeweza kuwaunganisha, raia wengi walipinga kurejea kwake, wakihoji nafasi yake katika utawala wa zamani na tuhuma ambazo hazijatatuliwa dhidi yake.

Katika miaka ya hivi karibuni, alijiepusha na shughuli ambazo zingelimfanya kuonekana hadharani mara kwa mara, hali ambayo inafanya taarifa za kifo chake kuwa zisizotarajiwa .

Kifo chake kinamaanisha nini kwa Libya

Mauaji ya Saif al-Islam Gaddaf yaondoa moja ya alama za mwisho za enzi ya utawala wa Gaddafi. Wachambuzi wanasema kifo chake hakiwezi kutatua mgawanyiko wa kisiasa nchini Libya lakini kinaweza kufunga ukurasa ambao umedumu tangu 2011.

Huku wachunguzi wakiwa mbioni kubaini waliohusika na kifo chake, tukio hilo linaangazia mapambano yanayoendelea nchini Libya dhidi ya uasi, malalamiko ambayo hayajatatuliwa, na urithi wa siku zake za nyuma zenye misukosuko.

Kwa baadhi ya Walibya, kifo cha Saif al-Islam ni alama ya mwisho wa mtu mwenye utata ambaye maisha yake yalionyesha kuinuka, kuanguka, vhini ya vivuli vya kudumu vya utawala wa baba yake Kanali Muamar Gaddafi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *