Chama cha ACT-Wazalendo nchini Tanzania, kimelaani mpango wa tume ya Uchaguzi wa Zanzibar (ZEC) wa kuchoma na kuteketeza nyaraka za Uchaguzi wa Oktoba 2025, uliofanyika visiwani humo.

Katika taarifa yake iliyotolewa Februari 4, 2026, chama hicho kimedai kuwa, kwa muda wa wiki mbili, kuanzia Januari 21, maombi ya chama hicho kisheria, ya kuiomba Mahakama itoe Amri kwa Tume ya Uchaguzi kuleta Mahkamani Nyaraka muhimu za uchaguzi kutokana na umuhimu wa nyaraka hizo katika kuamua Kesi zilizowasilishwa, yamekwama katika Ofisi ya Msajili wa Mahakama Kuu bila sababu za msingi.

“Baada ya tangazo la jana, sasa tumefahamu kwamba kumbe kuchelewa huku si kwa bahati mbaya; ni mkakati wa makusudi wa “kupunguza kasi ya utafutaji haki” ili kuipa nafasi ZEC kuchoma ushahidi wa kile kilichotokea kwenye vituo vya kupigia na kuhesabu kura,” kilidai chama hicho kupitia taarifa yake.

ACT-Wazalendo imesisitiza kuwa, ni kosa la jinai kuharibu ushahidi wakati kuna shauri la kisheria linaloendelea. 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *