VIWANJANI: “Unajua kuna changamoto ya muunganiko vilevile….”
Meneja wa klabu ya Simba Patrick Rweyemamu, amesema wanaelekea Angola wakiwa na kikosi cha wachezaji 23 huku wakiwa na maingizo ya wachezaji wapya ambao wanahitaji kuzoeana.
Meneja huyo ameongeza hawataathiriwa na matokeo yaliyopita, watarekebisha makosa ya michezo iliyopita na kuhakikisha wanashinda kaitka mchezo unaofuata.
Simba ipo safarini kwenda Luanda Angola kucheza dhidi ya Petro Atletico kwenye mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika.
Mechi itapigwa Februari 7, saa 1:00 usiku LIVE #AzamSports1HD
Imeandikwa na Katherini Shirima
Mhariri: @allymufti_tz
#CAFCL #LigiYaMabingwaAfrika